Kiswahili (Swahili)
Tenants Victoria ni huduma isiyolipishwa na ya siri kwa wapangaji. Ukurasa huu unakuambia jinsi tunavyoweza kukusaidia na jinsi ya kutuambia kuhusu tatizo lako la ukodishaji.
Jinsi gani tunaweza kukusaidia
Tenants Victoria hutoa taarifa na ushauri kusaidia wapangaji kutatua tatizo la kukodisha. Huduma zetu ni za bure na za siri.
Tenants Victoria inaweza:
- Kushauri kuhusu maswali maalum kama vile ukarabati (kutengenezwa) na ongezeko la kodi (kupandishwa kwa beyi ya kukodisha).
- Kuzungumuza kwa niaba yako na wamiliki wa nyumba au wakala wa mali isiyohamishwa (real estate agent)
- Kukusaidia au kukuwakilisha katika Victoria Civil and Administrative Tribunal (VICAT),
- Kutoa ushauri na msaada ikiwa unashida ya kulipa kodi, bili na madeni mengine
- Kukuunganisha na huduma nyingine za usaidizi.
Msaada tunaoweza kutoa unategemea:
- Aina ya shida ya kukodisha
- Una pesa ngapi
Jinsi ya kutuambia kuhusu shida lako la kukodisha
Ikiwa unakodisha nyumba yako kupitia mwenye nyumba ao wakala wa mali isiyohamishwa (real estate agent), tupigie kwa (03) 9416 2577.
Laini hii inafunguliwa Jumatatu, Jumanne, Alhamisi na Ijuma, 9.30am – 1.30 pm.
Takriban muda wa kusubiri ni zaidi ya dakika 40 kwa kutokana na mahitaji makubwa.
Ikiwa unakodisha nyumba yako kutoka kwa serikali au shirika la jamii, utupigie kwa 1800 068 860. Laini hii iko wazi Jumatatu hadi Ijuma, 9.00am – 4.00pm.
Ikiwa unaishi katika nyumba yenye kuwa na wapangaji wengi utupigie kwa 1800 068 860. Laini hii iko wazi Jumatatu hadi Ijuma, 9.00am – 4.00pm.
Je, naweza kuzungumuza kwa lugha yangu?
Ndiyo, ikiwa ungependa kuzungumuza kwa lugha yako mwenyewe, tutawasiliana na mkalimani kwa usaidizi.
Tutapanga kukupigia simu wakati ambapo mkalimani anapatikana
Tunatumia wakalimani waliioidhinishwa na National Accreditation Authority for Translators and Interpreters (NAATI).
Je, mtu anaweza kunipiga simu kwa niaba yangu?
Ndiyo. Mufanyakazi au msaidizi unayemwamini anaweza kutupigia simu. Ni bora zaidi ikiwa uko pamoja na mufanyakazi wako au mtu wa usaidizi wakati wanapiga simu.
Ni nini kinatokea unapowasiliana nasi?
Tutakuuliza maswali. Hii hutusaidia kuamua ni usaidizi gani tunaweza kukupa.
Kila kitu unachotuambia ni siri. Hatutamwambia mtu yeyote kile unachotuambia isipokuwa utuambie tunaweza.
Ikiwa hatuwezi kukusaidia, tunaweza kukupa maelezo ya mawasiliano na mtu ambaye anaweza. Hiki kinaweza kuwa kituo cha sheria cha jamii au shirika la kutoa huduma za jamii.
Maelezo zaidi kuhusu haki za kukodisha
Tovuti yetu ina habari kuhusu mada nyingi za kukodisha kwa Kiingereza.